Smartphone inayoruhusu ubadilishaji wa vipuli kwa urahisi

TEKNOLOJIA

Simu ya Fairphone ni simu janja ambayo ukishainunua haikupi ugumu tena kubadili kitu kama kamera, betri n.k, tena unaweza fanya mwenyewe.

Kampuni iliyopo nchini Uholanzi iliyoanzishwa mwaka 2010 inalenga kutengeneza simu janja ambayo mtumiaji wake ataweza kubadili na kununua vipuri vipya vilivyo bora au kubadilisha vilivyoharibika kwa urahisi.

simu ya fairphone

Simu hiyo inakuja na ‘screwdriver’ ya kukuwezesha kuifungua na kuweza kubadili vitu vingi ndani yake

Ukinunua simu yako utakuta ndani yake kuna vifaa vya kukusaidia kuifungua kwa urahisi na kubadili vitu kama vile kamera, betri, na vingine vingi ambavyo kwenye simu zingine ni vigumu kwa mtu kufanya mabadiliko hayo.

Lengo kuu ni kuhakikisha mtu anaweza kukaa na simu kwa muda mrefu bila ulazima wa kutumia pesa nyingi katika kununua simu mpya ili aweze tuu kupata kamera nzuri zaidi n.k.

Tayari kwa wastani watumiaji wa simu janja siku hizi wanakaa na simu kwa muda mrefu zaidi bila uhitaji wa kubadili simu na kupitia Fairphone lengo ni kufanya jambo liwe la kawaida na lenye manufaa kwa harakati za utunzaji mazingira.

fairphone

Kupitia tovuti yao watumiaji wanaweza kununua vipuli/part za simu hiyo kwa urahisi sana.

Sifa ya Fairphone 3 (toleo la sasa) linalouzwa kwa takribani Tsh Milioni 1.1 – 1.2 za kitanzania ni kama zifuatazo (ukishanunua bado una uwezo wa kuongeza uwezo mbalimbali kwa kununua vipuli vipya);

  • Programu endeshaji: Android 9, toleo safi la bila mbwembwe nyingi
  • Prosesa: Qualcomm Snapdragon 632 ikija na RAM ya GB 4
  • Diski Uhifadhi: GB 64 na ukiwa na uwezo wa kuoongeza kupitia eneo la microSD
  • Betri: mAH 3,000
  • Display: Full HD, inchi 5.65
  • Kamera: Megapixel 12, f/1.8, wakati kwa selfi ni Megapixel 8, f/2.0

Teknolojia zingine ni pamoja na uwezo wa 4G, laini mbili, Eneo la ulinzi wa utambuzi wa alama za vidole, na kitundu cha earphone.

Toleo la Fairphone 3 linakuja sokoni hivi karibuni na watu wanaweza kununua simu hiyo moja kwa moja kwenye tovuti yao na wao watatuma popote ulipo.

Mambo ya kuzingatia katika kuchaji simu na kufanya betri zidumu

TEKNOLOJIA

Kwenye kuchaji simu ni watu wengu wanafanya makosa mbalimbali ambayo yanasababisha mfumo wa kuchati au ata betri za simu zao kuharibika mapema. Leo fahamu mambo ya uzingatia katika kuchaji simu na kufanya betri zidumu.

Fahamu kwa kufuata baadhi ya haya maelezo kutahakikisha betri la simu yako haliwahi kuchoka – hii ikimaanisha uwezo wa kuchaji kwa haraka, na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu.

1. Usiwe unaacha simu yako iishe chaji hadi 0% kila saa

katika kuchaji simu

Mambo ya kuzingatia katika kuchaji simu: Usiache simu yako hadi iishe kabisa ndio uanze kuchaji

Kuisha kwa chaji hadi mwisho mara kwa mara kunaharibu uwezo wa betri la simu yako kukaa na chaji muda mrefu na pia kunaathiri kasi yake ya kuchaji haraka. Anza kuweka utaratibu wa kuchaji simu yako ikiwa kati ya asilimia 5 – 50%.

2. Kuacha simu yako kwenye chaji muda mrefu

Kuacha simu yako kwenye betri muda mrefu hasa pale ambapo imeshajaa inaharibu ubora wa betri la simu yako. Hii inahusisha wale wenye tabia ya kuweka simu kwenye chaji usiku kucha, kuweka simu kwenye chaji muda wote kazini n.k… hizi zote ni tabia zinazoua ubora wa betri la simu yako.

Kuacha simu ambayo ishajaa kwenye chaji inalazimisha betri kutengeneza joto jingi zaidi ya kawaida na hili linaharibu ubora wake.

3. Utumiaji wa chaja zisizokuwa na ubora

Kama umenunua simu kwa bei ya juu, ni bora pia uhakikishe unatumia chaja zenye kiwango cha juu. Chaja ambazo hazina ubora nje tuu ya kuchaji simu yako kwa utaratabu pia zinaweza kuharibu mfumo wa kuchaji simu yako (charging system).

4. Kuchaji simu yako wakati ina joto kali

Je simu yako ilikuwa eneo lenye joto kali? Iwe uliisahau eneo la dirishani au kwenye gari na matokeo yake simu kuwa ya moto usiiweke kwenye chaji hadi itakapopoa. Kuweka kwenye chaji na kufanya betri kupata umeme wakati lina joto kutasababisha betri kuanza kupoteza ubora wake.

Je ni wapi wewe umekuwa ukikosea zaidi?

Soma pia;

CC: TeknoKona

Hizi hapa simu mbili za Mara X na Z kutoka Rwanda

TEKNOLOJIA

Katika kuhakikisha kwamba jamii yake inapata teknolojia kwa bei nafuu zaidi Rwanda imekuwa nchi ya kwanza Afrika kuanzisha kiwanda cha utengenezaji simu janja unaohusisha utengenezaji wa vipuli vingi hapo hapo badala ya kuagiza nje.

Simu mbili tayari zimezinduliwa na muda mfupi zitaanza kupatikana katika masoko ya uuzwaji wa simu ndani ya Rwanda na katika nchi zingine za Afrika.

Simu hizo mbili zitafahamika kama Mara X na Mara Z ambazo zote zitakuwa zina uwezo wa kutumia laini mbili.

Rwanda wazindua simu janja mara rwanda

Kwa ufupi tumekuwekea uangalie sifa za simu hizo mbili kutoka Bara la Afrika.

Sifa za simu ya Mara Z

ProsesaQualcomm MSM8940 Snapdragon 435
Network2G, 3G, 4G
Ukubwa wa kioo5.7 inches, 720 x 1440 pixels, 18:9 aspect ratio, IPS LCD with   Corning® Gorilla® Glass and Oleophobic Coating.
Mfumo endeshi OSAndroid 8 Oreo.
Ukubwa wa uhifadhi32 GB
RAM3GB
Kamera ya Nyuma13 MP single camera, f2.0 Aperture, auto focus, Portrait Mode (Bokeh effect) , LED flash, 1080p@30fps video recording, Dual Recording.
Kamera ya Selfie13 MP, f2.2 Aperture, fixed focus, 1080p@30fps video capture.
Ujazo wa BetriLithium-Polymer 3070 mAh (Haichomoki)
FM RadioKuna redio

Muonekano wa Mara Z

Sifa zs simu ya Mara XINAYOHUSIANA  Brilliant: App Itakayo Kujulisha Kuwa Una Upeo Kiasi Gani!

ProsesaMediaTek MT 6739
Network4G LTE with VoLTE and ViLTE, VoWi-Fi
Ukubwa wa kioo5.5 inchi
Mfumo endeshi OSAndroid 8.1 Oreo GO Edition
Ukubwa wa uhifadhi16GB
RAM1GB
Kamera ya Nyuma13 MP
Kamera ya Selfie5 MP
Ujazo wa Betri3500mAh

Muonekano wa simu ya Mara X

CC: Teknokona

Wamiliki makundi ya WhatsApp watakiwa kuwa na Leseni

TEKNOLOJIA

Katika kudhibiti majukwaa ya mitandao ya kijamii, watawala nchini kenya wamependekeza muswada ambao utawalazimisha watu walioanzisha makundi ya WhatsApp, Facebook na Wanablogi kuwa na leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano ya Kenya.

Muswada huo ambao tayari umeshapelekwa Bungeni unataka Viongozi (Administrators) wa makundi ya WhatsApp kuwa na leseni na kuwasajili wanachama (Members) wa kundi na pia kujua anuani zao za mahala wanapoishi.

facebook whatsapp apps leseni za whatsapp

Na pia kuweka wazi kile kinachojadiliwa ndani ya kundi kwa jeshi la polisi. Kiongozi wa kundi atalazimika kujaza majina ya wanachama wake pamoja na anuani zao wakati wa kujaza fomu maalumu ya kupata leseni ya uendeshaji wa kundi lake.

Pia Viongozi hao watatakiwa wawe na wanachama waliofikia miaka 18 au zaidi.

Endapo muswada huo utapita basi yeyote atakayeendesha Kundi bila ya Leseni atakumbana na adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja Gerezani au faini ya Kshs 200,000/- (Takribani Tshs 400,000/- )

Aidha wanablogi watakaoendesha Blogu zao bila ya Leseni watapigwa faini ya Kshs 500,000 (Takribani 1,000,000/-) au kifungo cha miaka miwili gerezani.

Muswada huo unatarajiwa kusomwa Bungeni wiki ijayo.

cc: TeknoKona

5G Afrika Kusini

TEKNOLOJIA

5G yaanza kupatikana katika nchi ya kwanza Afrika. Baada ya ‘figisu figisu’ za mataifa ya Marekani na baadhi ya washirika wake wa ‘kuibania’ kampuni ya Huawei juu ya usambazaji wa teknolojia yake ya kisasa zaidi ya mtandao wa 5G, kampuni hiyo imepeleka teknoljia hiyo nchi ya Afrika Kusini.

5G Afrika Kusini

Inaonekana kwa Afrika kampuni hiyo haitapata vikwazo au ugumu katika biashara ukilinganisha na katika mataifa ya magharibi

Huawei kwa kushirikiana na kampuni inayotoa huduma za mawasiliano ya nchini Afrika Kusini ya RAIN, wamefanikiwa kuwezesha teknolojia ya mtandao wa 5G nchini humo.

Hatua hiyo inaifanya nchi ya Afrika Kusini kuwa nchi ya kwanza ya Bara la Afrika kuwa na teknolojia ya mtandao wa 5G ambao una kasi zaidi ya mara 10 ya mtandao wa 4G.

Awamu ya kwanza ya usambazaji wa teknolojia hiyo itahusisha miji miwili kabla ya kusambazwa nchi nzima.

Maeneo muhimu ya miji ya Johannesburg na Pretoria ndio itanufaika na awamu ya kwanza ya usambazaji wa 5G.

Mtandao huo wa 5G unatarajiwa kuwa na kasi ya MB 200 kwa sekunde mpaka MB 700 kwa sekunde.

Mkurugenzi Mtendaji wa RAIN, amesema amefurahishwa na hatua ya uzinduzi wa teknolojia ya 5G nchini humo hususani kampuni yake ikiweka rekodi ya kuwa mtandao wa kwanza wa kuanzisha huduma hiyo.

cc: TeknoKona

Toleo rasmi kwa mashabiki wa FC Barcelona (The Barca edition)

TEKNOLOJIA

Kama wewe ni shabiki kindakindaki wa timu ya FC Barcelona ya nchini Uhispania, Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition inaweza ikawa simu nzuri kwa ajili yako.

Oppo, kampuni ya utengenezaji simu ya nchini Uchina imetengeneza simu ambayo ni maalumu kwa mashabiki wa timu hiyo ya FC Barcelona.

Muonekano wake nje na ndani umepambwa kwa rangi zinazotumiwa na timu hiyo  Nyekundu na Buluu kuonesha uhalisia wa Barca ambao ni mabingwa wa La Liga.

Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition

Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition

Baadhi ya sifa za simu hiyo unaweza kuangalia hapo chini.

Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition.

Prosesa Qualcomm SDM855 Snapdragon 855
Network GSM / CDMA / HSPA / EVDO / LTE
Ukubwa wa Kioo 6.6 inches (1080×2340) (AMOLED)
Mfumo endeshi OS Android 9.0 (Pie)
Ukubwa wa uhifadhi 128GB, 8GB RAM
Kamera ya Nyuma 48-megapixel (f/1.7) + 13-megapixel (f/3.0) + 8-megapixel (f/2.2)
Kamera ya Selfie16-megapixel (f/2.0)
ujazo wa Betri Li-Po 4065 mAh (Haichomoki)
oppo

Kampuni ya Oppo ambayo ni sehemu ya wadhamini wa timu ya FC Barcelona imeanza kuuza simu hiyo mwishoni mwa mwezi Julai katika nchi ya China, Spain, India, Holand, France na baadhi ya nchi za Ulaya.

Copyright: Teknokona

Je, kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A?

TEKNOLOJIA

Je ushawahi kujiuliza kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A kwenye kompyuta zinazotumia Windows? Leo fahamu.

Kwa watumiaji wa kompyuta wa tokea miaka ya 90 ni rahisi wao kuelewa sababu, au kutojua sababu ila washawahi kutumia kompyuta wakati diski zinatambulika pia kwa namba A.

Historia

  • Programu endeshaji ya Windows ilitengenezwa juu ya mfumo endeshaji mwingine wa kwanza kutoka Microsoft uliokuwa unatambulika kwa jina la MS-DOS. Kipindi hicho mfumo wa diski za flopi ndio zilikuwa zinatumika (floppy drives).Je kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A?: Muonekano wa diski za Flopi
  • Katika kompyuta hizo kompyuta ilikuwa ina uwezo wa kutumia hadi diski za flopi mbili kwa wakati mmoja na hivyo moja kwa moja ya kwanza ilichukua nafasi ya utambulisho wa A: na ya pili ikachukua nafasi ya utambulisho wa B:.

Baadae diski za mfumo wa ‘harddrives’ zilivyokuja ndio zikachukua nafasi ya C:, na mgawanyo wa diski (partition) wa pili au diski nyingine ndani yake ndio ikachukua nafasi ya D:, sehemu ya cd, yaani CD-ROM ndio ikapewa nafasi ya E:

diski za flopi Je kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A?

Hiyo ndio historia fupi na sababu kuu kwa nini diski kwenye kompyuta yako kwa sasa zinaanza na kubeba namba C:, ila kumbuka teknolojia ya utambuzi wa diski za flopi bado upo kwenye Windows. Mfano ukiwa na kimashine cha kutumia flopi na ukakipachika kwenye kompyuta yako basi flopi itatambulika kwenye Windows na itachukua namba A:

Copyright: Teknokona

Apps za WhatsApp na Instagram kufanyiwa mabadiliko ya majina

TEKNOLOJIA
apps za whatsapp na instagram

Apps za WhatsApp na Instagram ambazo zinamilikiwa na kampuni ya Facebook, zipo njiani kufanyiwa mabadiliko ya majina.

Inasemekana uamuzi huu umelazimika kufanyika kutokana na mashambulizi/malalamiko ya makampuni mengine kuhusu ukiritimba (monopoly) wa Facebook.

Apps hizi tatu zinaongeza kwa wingi wa watumiaji katika eneo la kuchati kwenye masoko yote ya apps: watumiaji wa Android na iOS

Makampuni shindani yameshalalamika kwa muda mrefu kwa taasisi za ushindani wakisema ni vigumu kwa mtumiaji kufahamu kama apps za WhatsApp na Instagram zinamilikiwa na Facebook, na kama watumiaji wakielewa hili linaweza kuwafanya wasikubali kutumia na kuipa data zao nyingi kampuni moja tuu – yaani Facebook.

Kutokana na hilo Facebook wamesema wapo njiani kuboresha majina ya apps hizo; mabadiliko hayo yanamaanisha app ya Instagram itafahamika kwa jina la Instagram from Facebook,- yaani Instagram kutoka kwa Facebook, na WhatsApp ikiwa ni WhatsApp from Facebook – yaani WhatsApp kutoka kwa Facebook.

Lengo kuu hapa ni kuweka wazi kwa watumiaji ya kwamba app wanayotaka kuipakua inatoka kwa kampuni ya Facebook.

Facebook wamesema ila bado ingawa majina hayo yataonekana sehemu zote, hii ikiwa ni pamoja na kwenye masoko ya apps, ila kwenye simu yako baada ya kuipakua majina haya mapya hayataonekana kwenye eneo la apps zilizo kwenye simu yako – bado apps zitaandikwa kwa jina fupi, yaani WhatsApp na Instagram. Hii ni kwa sababu majina mapya ni marefu sana. Majina mapya yatatumika sehemu zingine zote.

Pia uamuzi huu umekuja katika kipindi ambacho tayari Facebook wamesema wamewekeza katika utafiti wa kuunganisha apps hizi maarufu katika eneo la kuchati. Yaani mtumiaji wa Instagram aweze kumtumia ujumbe utakaokwenda WhatsApp, na mtu kupitia WhatsApp aweze kuchati na mtu anayetumia Messenger (Facebook). Muunganisho huu wa huduma ya kuchati upo katika matengenezo kwa sasa.

Copyright: Teknokona

Huawei bila apps za Google

TEKNOLOJIA

Kampuni ya Huawei yatambulisha rasmi toleo lao la simu janja za hadhi ya juu za Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro, ingawa zinakuja na teknolojia za kisasa hii ikiwa ni pamoja na 5G ila haziji na uwezo wa kuwa na apps maarufu za Google.

Kupitia simu zake hizi mpya za Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro itakuwa ni nafasi ya Huawei kujipima uwezo wao kama wanaweza kuendelea kutishia soko la simu janja za hadhi ya juu bila simu hizo kuja na familia ya apps za Google.

Kutokana na katazo la kibiashara liliwekwa na serikali ya Marekani kwa makampuni ya nchini humo, Google, Microsoft, Facebook na makampuni mengine mengi yaliyokuwa yakifanya biashara na Huawei yamejikuta yakikata uhusiano huo na hivyo kuzuia huduma zao kupatiakana kwenye simu au kompyuta mpya zinazotengenezwa na Huawei.

Huawei mate 30

Je simu hii inakosa vipi vikubwa?

>Apps

Simu hizi zinakuja bila apps maarufu kama vile Google Playstore, Google Maps, Google Chrome, na zingine mbalimbali zinazomilikiwa na Google.

>Updates/Masasisho ya Google

Simu hii haitakuwa inapata masasisho muhimu ya kiusalama kwa wakati ukilinganisha na makampuni yanayokuja na toleo la Android kutoka Google. Kawaida inaweza kuchukua miezi kadhaa kabla ya masasisho ya kiusalama yaliyotengenezwa na Google kufikia toleo la bure la Android – ambalo ndilo Huawei anatumia kwa sasa.

>Kutokuwa na GMS (Google Mobile Services)

GMS – Google Mobile Services, ni teknolojia inayojumuhisha mfumo mzima wa kutumia teknolojia za kimawasiliano ndani ya simu. Kupitia teknolojia hii basi apps zinaweza kutumia vizuri teknolojia za mawasiliano zilizowekwa kwenye simu husika. Ata simu za China ambazo zimekuwa zikitengenezwa na kuuzwa nchini humo bila apps za Google bado zimekuwa zikitumia GMS ndani yake. Na hili limekuwa likifanya kuwa rahisi simu hizi kuwekwa apps za Google zikiuzwa nje ya China.

Simu za Huawei kuanzia sasa ikiwa ni pamoja na Mate 30 zinakuja na mfumo wa HMS – Huawei Mobile Services. Suala hili lina maanisha ata kama ukijaribu kuweka apps za Google kwa lazima – kwa kulazimisha kuweka Google Services (mfumo wa huduma za Google) bado itashindikana kwa kuwa mfumo huo unaohitajika kwa ajili ya apps za Google kufanya kazi hauendani na ule mfumo wa teknolojia mama ya kwenye programu endeshaji (yaani HMS).

Kutokana na hili ndoto ya simu hiyo kuweza kutumia apps za Google isahau.

simu za huawei mate 30 na mate 30 pro

Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro

Je soko la app la Huawei lina apps ngapi?

Kwenye simu hii kwa sasa bado kutakuwa na apps chache sana ukilinganisha na simu za Android ya Google. Hadi sasa soko la apps la kwenye simu hiyo lina apps 45,000 ukilinganisha soko la Google Playstore lina zaidi ya apps milioni 2.7.

Huawei wameweka bajeti kubwa kuwavutia watengenezaji apps kuhakikisha mfumo wake wa HMS unatambuliwa na apps zao ili ziweze kufanya kazi kwenye simu zake pia.

Sifa na uwezo wa Huawei Mate 30

huawei mate 30
  • Inchi 6.53 OLED display
  • Prosesa Kirin 990 CPU
  • Uwezo wa kuzuia maji (water resistance)
  • Kamera ina lensi tatu – megapixel 40, 16 na 8.
  • Kamera ya selfi ni ya megapixel 24
  • Uzito wa gramu 198 grams, na upana wa mm 8.8
  • Betri la mAh 4,200
  • Uwezo wa kuchaji wa bila waya (wireless charging).
  • Programu endeshaji ya Android 10 (toleo la bure – open source)
  • RAM ya GB 8, na diski ujazo wa GB 128.

Huawei Mate 30 Pro

Mate 30 Pro
  • Inchi 6.62 OLED display
  • Prosesa Kirin 990 CPU, 16-core Mali G76 GPU
  • Uwezo wa kuzuia maji (water resistance)
  • Kamera ya lensi tatu, hii ikiwa ni ya Megapixel 40, 40, 8.
  • Kamera ya selfi ni ya megapixel 32- inasaidiwa na teknolojia ya kuboresha picha (AI HDR)
  • Uzito wa gramu 198 grams, na upana wa mm 8.8
  • Betri la mAh 4,500
  • Uwezo wa kuchaji wa bila waya (wireless charging) na pamoja na kuweza kuchaji vifaa vingine kwa kutumia teknolojia hiyo.
  • Programu endeshaji ya Android 10 (toleo la bure – open source)
  • RAM ya GB 8, na diski ujazo wa GB 256, ila pia kuna uwezekano wa toleo la GB 512 kuja pia.

Simu zote zinakuja pia na teknolojia za USB Type C, mfumo wa mwasiliano wa 5G, uwezo wa kutumia Memori Kadi, na teknolojia zingine muhimu zilizozoeleka katika simu janja za kisasa.

Bei:

Huawei Mate 30 Pro itauzwa kwa $1,200, takribani Tsh 2,800,000/= huku Huawei Mate 30 ikienda kwa bei ya Tsh 2,000,000/=. Bei zitapanda kulingana na ujazo zaidi.

Copyright: teknokona